Waziri Lukuvu awabananisha wadaiwa sugu wa Ardhi, wamo wakuu wa taasisi, mashirika na makampuni, Serikali yadai zaidi Bilioni 200 (+ Video)

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, William Lukuvu akizungumza na wakuu wa taasisi, mashirika na makampuni takribani 207 yanayodaiwa kodi ya pango la ardhi ambapo Serikali inadai zaidi ya Shilingi bilioni 200 za kodi yake ya ardhi.

Katika mashirika hayo yote yaliyotajwa TTCl inaongoza kwa kuwa na deni kubwa ikidaiwa zaidi ya shilingi bilioni 40 ya kodi ya ardhi ikifuatiwa na TANESCO ambayo inadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 25.

Katika hotuba yake, Waziri Lukuvi amesema wadaiwa wote hao watatakiwa kulipa kodi hiyo kabla ya Juni 20 na mwisho wa zoezi la kulipa madeni hayo ni Novemba ili kuepuka hatua za kisheria zitakazochukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwakamata na kutaifisha mali zao.

The post Waziri Lukuvu awabananisha wadaiwa sugu wa Ardhi, wamo wakuu wa taasisi, mashirika na makampuni, Serikali yadai zaidi Bilioni 200 (+ Video) appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *