Wazazi waombwa wapunguze mahari, Yaelezwa kuwa kitendo hicho kitaondoa woga kwa vijana wa kiume

Wazazi nchini Tanzania wameombwa kupunguza mahari za mabinti wao, Ili kuondoa kikazo kwa wanaume wenye lengo la kuoa lakini wanakwamishwa na vukubwa wa vikwazo vya mahari.

Image result for watoto wa kike mahari

Ombi hilo limetolewa visiwani Zanzibar na mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Bi. Asha Suleiman Iddi katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya Qaswida.

Nawashauri na kuwaasa wazazi wenzangu, msiwatumie vijana wenu wa kike kama chanzo cha mapato. Mnawawekea mahari kubwa sana, mnasababisha vijana wakiume washindwe na waogope kujitokeza kuwaona,“.amesema Bi. Asha.

Zanzibar na maeneo mengine ya Kanda ya ziwa Tanzania Bara, ni moja ya maeneo yenye wazazi wanaotoza mahari kubwa kwa watoto wao wa kike.

The post Wazazi waombwa wapunguze mahari, Yaelezwa kuwa kitendo hicho kitaondoa woga kwa vijana wa kiume appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *