Timu nne za Tanzania kushiriki michuano ya CAF 2020, ni klabu bingwa na Shirikisho Afrika

Ifikapo mwaka 2020 Tanzania itawakilishwa na jumla ya klabu nne kwenye michuano mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Klabu mbili zitashiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika na nyingine mbili kwenye kombe la Shirikisho Afrika, michuano yote hii inayomimamiwa na Shirikisho la soka Afrika CAF.

Hii si kawaida kwa Tanzania lakini nafasi hiyo imepatikana kutokana na wawikili wa Tanzania Simba SC kufanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano hiyo, kwakufika hatua ya robo fainali kabla ya kutolewa na TP Mazembe.

Kanuni zinasema kuwa nchi itakayofikisha pointi 12 katika msimu kama huu unaoukaribia kuumaliza basi msimu wa pili baada ya kwisha ule ulioifikisha nchi yenu alama 12 zilizotokana na kufanya vema kwa klabu zenu zitapata nafasi ya kuingiza klabu nne katika michuano hiyo inayoandaliwa na CAF.

Kutokana na Simba kufika hatua hiyo ya robo fainali imeifanya Tanzania kufikisha jumla ya pointi 18 huku Tanzania ikipanda hadi nafasi ya 12 ya ubora wa vilabu barani Afrika (ranks).

Pointi tatu kati ya hizo 18 zikitokana na Yanga kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho katika msimu wa mwaka 2016 na 2018.

Kufuzu kwa Simba robo fainali msimu huu, kumeipatia Tanzania pointi 15 ambapo zikichanganywa na zile 3 za Yanga, inakuwa na pointi 18.

Kufuzu kwenye hatua ya makundi ni pointi 0.5 na kufika robo fainali ni pointi 3. Simba imefika robo fainali msimu huu 2018/19 ambao thamani yake ni pointi 5. Maana yake ni 3×5=15.

Pointi hizi 15 zikijumlishwa na zile 3 za Yanga, Tanzania inakuwa na pointi 18. Hata hivyo pointi hizi zitaingia kwenye mahesabu kuanzia msimu ujao kwa ajili ya matumizi ya msimu wa mbele yake, yaani 2020/2021

The Countries 

1– Morocco 133*
2-Tunisia. 129*
3-Egypt. 105*
4-Algeria 92*
5-DR Congo. 82*
6- S.Africa. 71.5*
7-Zambia. 40.5*
8-Sudan. 35*
9- Nigeria. 32.5
10- Guinea 30*
11- Angola 21.51

12-Tanzania 18*

13- Ivory Coast 15
14-Kenya 14*
15 -Mozambique 13
16-Congo 11.5
17-Uganda 11
18-Libya 10 
19- Ghana 9
20-Rwanda 8

Club rankings 
Top 25
1-TP Mazembe
2-Al Ahly
3-Wydad
4-Esperance
5-Etoile du Sahel
6-Sudan
7-Horoya
8-Zamalek
9-USM Alger
10-Raja 
11-Zesco
12-AS Vita
13- Al Hilal
14-Club Africain
15-Entente Setif
16-RS Berkane
17-CS Sfaxien
18-Petro Luanda
19-Enyimba
20-CS Constantine
21-FUS Rabat
22- Simba
23-Gor Mahia
24- Orlando Pirates
25-Supersport
26-Asec Mimosa
27-JS Saoura
28-MC Alger
29- Al Ahly Tripoli
30-Al Merreikh

The post Timu nne za Tanzania kushiriki michuano ya CAF 2020, ni klabu bingwa na Shirikisho Afrika appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *