Shirika la Msalaba Mwekundu latoa sababu za kuwatafuta wafanyakazi wake waliotekwa na kundi la IS Syria miaka 5 iliyopita

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kuwa linafuatilia taarifa za wafanyakazi wake watatu ambao walitekwa na kundi la Islamic State IS Nchini Syria miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa BBC. Wafanyakazi wa shirika hilo waliotekwa ni Louisa Akavi, Alaa Rajab na Nabil Bakdounes walitekwa Oktoba 2013 walipokuwa wakisafiri jimbo la Idlib kaskazini mwa Syria.

Taarifa za kuaminika zinaeleza kwamba Bi. Louisa Akavi alikuwa hai hadi mwaka 2018 akiwa mikononi mwa kundi hilo la IS. Huku Alaa Rajab na Nabil Bakdounes ikiwa haijulikani kama wapo hai ama la.

Bi Akavi, ambaye ni rais wa New Zealand, mwenye umri wa miaka 62 ni muuguzi ambaye alifanya kazi kwa miaka 17 katika maeneo ya kutoa misaada.

Alaa Rajab na Nabil Bakdounes, wote wawili ni raia wa Syria waliokuwa madereva na waliofanya kazi ya kutoa misaada ya kibinadam nchini humo.

New Zealand inasema kuwa kikosi maalumu cha jeshi kimekuwa kikijaribu kutafiti ili kujua ni wapi alipo Bi.Akavi.

Mmoja wa mateka wa Msalaba mwekundu aliyetekwa na IS

Hata hivyo wasiwasi umezidi kuongezeka iwapo Bi.Akavi atapatikana kufuatia kusambaratika kwa ngome ya mwisho ya wapiganaji wa IS mwezi uliopita karibu na mpaka wa Iraq.

Bi .Louisa Akavi ni mzoefu kufanya kazi katika maeneo ya mizozo kwani kabla ya kutekwa kwake alikwisha fanya kazi nchini Bosnia, Somalia, na Afghanistan.

Alinusurika katika shambulizi la mwaka 1996 lililolenga kambi ya wafanyakazi wa Msalaba mwekundu kule Chechnya,ambapo watu sita waliuawa. Mwaka 1999 alitunukiwa tuzo ya Florence Nightingale kwa kazi yake ya uuguzi.

By Ally Juma.

The post Shirika la Msalaba Mwekundu latoa sababu za kuwatafuta wafanyakazi wake waliotekwa na kundi la IS Syria miaka 5 iliyopita appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *