Serikali yatoa tamko juu ya tukio la kukamatwa kwa wanahabari na viongozi wa CPJ

Baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Vyombo vya Dola kushirikiana na idara ya Uhamiaji, vinawashikilia Wanaharakati wawili wa Kamati Maalum ya Kuwalinda Wanahabari duniani (CPJ ) walioitembelea Tanzania mapema jana, hatmaye serikali imetoa tamko.

Tamko lililotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter, imeeleza kuwa Ofisi yake imezipata taarifa hizo na itafuatilia kwa karibu tukio hilo.

“Ofisi yangu inafuatilia kujua kwa nini wanaoitwa waandishi wa habari wa CPJ waliruhusiwa kuingia nchini lakini baadaye wakalazimika kuhojiwa na uhamiaji na kuachiwa.”imeeleza taarifa.

Kwa maelezo ya Msemaji Mkuu wa Serikali, inaonesha kuwa viongozi hao mpaka sasa tayari wameachiwa huru.

Mapema leo Kamati ya CPJ ilitoa taarifa hiyo ya kukamatwa kwa Kiongozi Mkuu wa Kamati hiyo Afrika, Angela Quintal sambamba na Muthoki Mumo ambaye ni Mwakilishi wa Afrika Mashariki, na kuitaka Serikali ya Tanzania iwaachie mara moja watu hao.

Taarifa hiyo iliyotolewa na CPJ imeeleza kuwa Viongozi wao walikamatwa na Maafisa waliojitambulisha kuwa wanatoka Idara ya Uhamiaj wakiwa katika Hoteli waliyofikia jijini Dar es Salaam jana.

The post Serikali yatoa tamko juu ya tukio la kukamatwa kwa wanahabari na viongozi wa CPJ appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *