Rich Mavoko awashukuru BASATA kwa kupokea malalamiko yake na WCB ‘hata iweje nyie ndio walezi wa sanaa yetu’

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Rich Mavoko amejitokeza kwa mara ya kwanza kuelezea sakata la kukutana na BASATA kuwasilisha mkataba wake aliosaini na WCB aliodai kuwa unamkandamiza.

Rich Mavoko

Mavoko kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa anashukuru kukutana na BASATA na kupata elimu ya kutosha huku akiwamwagia sifa kuwa hao ndio maana halisi ya walezi wa sanaa yetu nchini Tanzania.

Leo Alhamisi Agosti 9, 2018 Rich Mavoko amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza ambapo amepeleka mkataba wake na WCB akidai uangaliwe upya kwani umekuwa ni wa unyonyaji.

The post Rich Mavoko awashukuru BASATA kwa kupokea malalamiko yake na WCB ‘hata iweje nyie ndio walezi wa sanaa yetu’ appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *