RC Makonda anukuliwa vibaya kuwa Mo Dewij amepatikana (+Video)

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda amekanusha zile taarifa zinazoenea kwenye vyombo vya habari kuwa Mfanya biashara mkubwa kutoka Tanzania Mo Dewij aliyetekwa asubuhi ya leo na watu wasiojulikana amepatikana. Makonda amesema “Yeye hakuongea taarifa kama zile na wale waliozieneza taarifa hizi wakanushe mapema iwezekanavyo”

Hadi hivi sasa uataratibu wa kumtafuta mfanyabiashara huyo bado unaendelea na jeshi la Polisi ndio linashughulikia suala hilo.lakini pia amewataka wananchi wa mkoa wa Dar Es Salaama kuonyesha ushirikiano na jeshi la Polisi kama kuna mtu anajua chochote basi atoe taarifa na kama hujui basi ukae kimya usije anza kueneza taarifa zisizo na uhakika.

By Ally Juma

The post RC Makonda anukuliwa vibaya kuwa Mo Dewij amepatikana (+Video) appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *