Nikki Mbishi amtolea uvivu Fid Q kisa CD ya album yake, adai wataendelea kuzikana japo amemdharau

Rapper Nikki Mbishi ambaye siku zote huwa hakai na jambo moyoni ameamua kuweka hisia zake wazi kwa kumchana mkongwe, Fid Q kuwa amemkosea kwa kugawa nakala ya Album yake ya Sam Magoli bure ile hali alimpa kwa heshima yake.

Image result for nikki mbishi
Nikki Mbishi

Nikki amesema kuwa kitendo hicho kimemuumiza sana kwani mtu aliyempa hakuwa na Interest yoyote na Album yake jambo ambalo ameona kama Fid Q kaichukulia poa Album yake.

Sikuelewa maana ya kukupatia copy ya album yangu na wewe ukagawa kwa yule jamaa halafu BURE tena kwa mtu ambaye hakuwa hata na INTEREST,ni bora ningebaki na CD yangu,maana nilikupa kwa HESHIMA ila nikaona umeichukulia poa.. @FidQ,”ameandika Nikki kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kwenye moja ya comments ya Tweet hiyo, rapper mwenzie Wakazi alitoa mtazamo wake kwa kuandikaAmekukosea sana… I hope there’s a solid reason behind it. Labda ulikuwa umemuudhi hapo nyuma, akawa ameshikilia hisia ngumu.“.

Naye Nikki Mbishi akajibu kwa ufupi kwa kuandika “Sio mbaya sana japo ilinipa ukakasi kidogo….Tuendelee KUZIKANA.”.

Hata hivyo, Fid Q hajajibu tuhuma hizo za Nikki Mbishi sababu hasa ya kufanya hivyo.


The post Nikki Mbishi amtolea uvivu Fid Q kisa CD ya album yake, adai wataendelea kuzikana japo amemdharau appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *