Mzimu wa Ole Gunnar waendelea kuitafuna PSG, baada ya Neymar sasa zamu ya Cavani kuikosa Manchester United UEFA

Edinson Cavani huenda akakosa mechi ya mkondo wa kwanza ya vilabu bingwa dhidi ya Manchester United. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anauguza jeraha katika kiuno chake baada ya kufunga mkwaju wa penalti katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Bordeaux. Mshambuliaji mwenza Neymar hatoshiriki katika mkondo wa kwanza wa mechi hiyo na ule wa pili mnamo tarehe 6 mwezi Machi.

Kwa mujibu wa BBC. Katika taarifa PSG imesema kuwa kutopatikana kwa Cavani kutategemea jeraha lake katika siku chache zijazo. Akizungumza na runinga ya Ufaransa siku ya Jumapili, mkufunzi Thomas Tuchel alisema: Hakuna habari nzuri kuhusu Edi hii leo.

Aliongezea: Anafanyiwa vipimo hii leo katika kituo cha mazoezi, klabu itatoa taarifa baadaye , lakini kwa maoni yangu habari hizo haziridhishi. Itakuwa vigumu sana kumchezesha.

Kuna matumaini ya kiwango cha chini sana. Tuna matumaini lakini vipimo vya kwanza sio vizuri.

Mshambuliaji wa Brazil Neymar alipata jeraha katika ushindi wa 2-0 dhidi ya mabingwa wa kombe la ligi nchini Ufaransa Strasbourg tarehe 23 Januari na hatoweza kucheza kwa wiki 10.

Hatua hiyo inamwacha mshindi wa kombe la dunia Kylian Mbappe-ambaye alichukua mahala pake Cavani wikendi iliopita.

Hatahivyo, Tuchel alisema kuwa kulikuwa na habari njema kwa mchezaji mwengine muhimu Marco Verratti, ambaye alishiriki katika mechi dhidi ya Bordeaux baada ya kukaa nje kwa wiki tatu na jeraha la kifundo cha mguu.

“Verratti anaweza kucheza na atacheza, alisema raia huyo wa Ujerumani . Nina wasiwasi kwasababu wachezaji muhimu wanauguza majeraha” .

Kwa mechi kuu katika kombe la vilabu bingwa ni muhimu kuwa na wachezaji muhimu wenye uzoefu mwingi.

PSG iko pointi 13 juu ya ligi ya daraja la kwanza lakini ushindi wao dhidi ya Bordeaux ulijiri baada ya wiki ngumu .

By Ally Juma.

The post Mzimu wa Ole Gunnar waendelea kuitafuna PSG, baada ya Neymar sasa zamu ya Cavani kuikosa Manchester United UEFA appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *