Msimu wa 7 wa tuzo za ‘Africa Magic Viewers’ Choice Awards 2019 wafunguliwa rasmi (+Video)

Jumatatu Disemba 2, 2019. Baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye Africa Magic kwa kushirikiana na kampuni ya MultiChoice Africa, imetangaza rasmi kupokea maombi ya kushiriki kwenye msimu wa saba (7) tuzo za Kimataifa za African Magic Viewers’Choice Awards 2019 maarufu kama AMVCA Awards.

Akizungumza wakati wa kutangaza rasmi ufunguzi wa tuzo hizo kwa msimu huu wa saba, Mkuu wa Uhusiano wa Kampuni ya MultiChhoice Tanzania Bw. Johnso Mshana amesema kuwa, ”Tuzo hizi ni mahususi kwa ajili ya filamu za Afrika na hufanyika kila mwaka ili kutambua jitihada kubwa za watengenezaji filamu, waigizaji pamoja na mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika sekta hii ndani ya mwaka husika,” alisema Mshana.

Johnso Mshana ameongeza, ”Hivyo nitoe rai yangu kwa magwiji wote wa filamu Tanzania kuweza kutumia fursa hii adimu kuweza kushiriki katika mchakato huu ambao utawezesha kujitangaza na kuzitangaza kazi zinazotengenezwa hapa nyumbani katika nyanja za Kimataifa kupitia tuzo hizi.”

Maandalizi kwaajili ya msimu huu wa saba yanaendelea na tuzo hizi zitafanyika mnamo mwezi Machi mwaka 2020 ili kuwapata vinara mbalimbali wa filamu kutoka barani Afrika.

Maombi yanayokaribishwa kwa ajili ya kushiriki ni ya kazi za filamu na televisheni ambazo zilitayarishwa na kuoneshwa kuanzia April 1, 2018 hadi Novemba 30, 2019.

UFUATAO NI MWONGOZO WA JINSI YA KUTUMA KAZI KWA AJILI YA KUSHIRIKI

Hatua ya 1: Andaa Clip ya dakika 5 (reel) kwa ajili ya online Submission.

Hatua ya 2: Ingia kwenye tovuti ya Africa Magic kupitia www.africamagic.tv/AMVCA na Click kwenye banner ya AMVCA Seventh edition itakayokupelekea kwenye ukurasa wa kutuma maombi

Hatua ya 3: Jaza fomu za kuomba kushiriki halafu Upload Clip yako. Kila online Submission iliyokamilika itapewa namba ya kumbukumbu kuthibitisha

Hatua ya 4: Hakikisha Video ya kazi yako ina uzito usiozidi MB 300

Hatua ya 5: Weka namba yako ya kumbukumbu, kisha tuma Hard drive ya kazi uliyoiwasilisha mtandaoni kwenda:

Margaret Mathore

2nd floor, MNET offices

Local Production Studio

Jamhuri Grounds off Ngong road

Nairobi Kenya

Kwa maelezo zaidi wasiliana: Johnson.mshana@tz.multichoice.com / grace.mgaya@tz.multichoice.co

The post Msimu wa 7 wa tuzo za ‘Africa Magic Viewers’ Choice Awards 2019 wafunguliwa rasmi (+Video) appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *