Kamanda Mambosasa awataja waliohusika kumteka mfanyabiashara mkubwa Tanzania Mo Dewij (+Video)

Taarifa kubwa kabisa zilizoenea kwa sasa ni zile kuwa mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji maarufu kama Mo Dewji ,ametekwa leo alfajiri wakati alipokuwa akielekea mazoezini. Kwamujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Mo alifika katika hoteli moja ya kifahari katika eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam kama ilivyo ada yake kila siku alfajiri kwaajili ya kufanya mazoezi ya viungo.

Hatahivyo, punde aliposhuka tu kwenye gari yake, watu wasiofahamika walijitokeza na kufyatua risasi hewani kisha kumnyakua mfanyabiashara huyo na kutokomea nae kwenye gari lao.

Kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amezungumza na vyombo vya habari na kusema kuwa “wamepata taarifa hiyo na wanaifuatilia ingawa waliohusika na utekaji huo wakitajwa kuwa ni wazungu wawili ambao walijifunika nyuso zaona kunvamia wakati anashuka na kufanikiwa kutekeleza tukio hilo ingawa madhumuni ya utekaji bado hatujayajua”

By Ally Juma.

The post Kamanda Mambosasa awataja waliohusika kumteka mfanyabiashara mkubwa Tanzania Mo Dewij (+Video) appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *