Joti afunguka kuwa anaweza kuigiza filamu yoyote pia ameeleza hali ya kiafya ya Vengu ” Bado anaumwa” (+Video)

Mchekesha maarufu kutoka hapa nchini bwana Lucas Mhuvile alimaarufu kwa jina la kisanii Joti amefunguka mwanzo mwisho kuhusiana na Tamthilia yao ya Mwantumu ambayo inatarajiwa kuanza siku ya jumanne octoba 16 kupitia Chaneli ya DStv ya Maisha Magic Bongo ambayo itakuwa inaonyeshwa mara mbili kwa wiki yaani siku za Jumanne na Jumatano muda wa saa moja na nusu usiku.

Mchekeshaji huyo ameweza kuigiza katika vipengele vitatu (Scene) katika tamthilia ya Mwantumu msimu mpya wa pili ambapo ameelezea kunaptikana vipengele zaidi ya 19.

Joti akiigiza katika tamthilia hiyo ameweza kuvaa uhusika wa watu watatu,mtu wa kwanza akicheza kama Mzee Mrisho, pia akiigiza kama Kabomba na ya tatu akicheza kama Mwantumu Sahare.

Akiongea na Bongo five Joti amesema kuwa ” Yeye anaweza kuigiza katika tamthilia yoyote na pia na mtu yoyote na mahala popote pale mahala atakapowekwa na hapo kinachoonekana ni uwezo”

Lakini pia mchekeshaji huyo hakuishia hapo aliweza kuiongelea hali ya kifya ya mchekeshaji mwenzake ambaye ni Vengu na kusema kuwa “Jamaa bado anaumwa na tumuombee sanaa ingawa kwa maendeleo ya daktari hali yake inaenda kuwa nzuri”

Alipoulizwa kuhusu kinachomsumbua alikataa kuongea na kusema kuwa ” Mimi sio msemaji kwa maana kuwa mimi sio daktari wa sio msemaji wa familia mimi ni kama muigizaji mwenzake na mwanafamilia tu ila sio msemaji cha msingi jamaa bado anaumwa”

Mbali na hilo msanii huyo amefunguka na kuiomba Serikali “Iandae mazingira ya kuwakumbuka wasanii wakubwa ambayo wameacha alama katika nchi yetu kwa wamekuwa kioo kwa jamii la watu hawauoni msaada wao” huku akimtolea mfano marehemu mzee Majuto.

By Ally Juma.

 

The post Joti afunguka kuwa anaweza kuigiza filamu yoyote pia ameeleza hali ya kiafya ya Vengu ” Bado anaumwa” (+Video) appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *