Hivi ndivyo Rais Magufuli alivyomjibu RC Makonda, baada ya kusema anataka kuwa kama Rais Magufuli kwenye utendaji wa kazi (+ Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli , jana katika hafla ya kupokea Ndege mpya aina ya Airbus A220-300, ambayo itakuwa Ndege ya pili ya aina hiyo kutua Tanzania na Tanzania kuwa ndio nchi ya kwanza barani Afrika kumiliki aina hiyo ya Ndege, aliweza kumjibu Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh. Paul Makonda.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda aliwaomba viongozi wa dini wamuombee ili akikua awe kama Rais Magufuli katika utendaji kazi na hekima zake. Baadaye Rais aliweza kumjibu Makonda na kusema ” Nataka uwe zaidi yangu”

By Ally Juma.

The post Hivi ndivyo Rais Magufuli alivyomjibu RC Makonda, baada ya kusema anataka kuwa kama Rais Magufuli kwenye utendaji wa kazi (+ Video) appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *