Harmonize aiokoa Ndanda SC baada ya kukwama Singida kisa pesa za hotel

Msanii wa bongo fleva Harmonize ambaye pia ni shabiki mkubwa wa timu ya Ndanda SC, ametoa shilingi milioni 3.5 kwaajili ya kuisaidia timu hiyo iliyokwama mkoani Singida baada ya mchezo wake wa LigikuuTanzaniaBara uliochezwa Oktoba 6, 2018 dhidi ya Singida United, na kufungwa mabao 3-1.

Timu hiyo ilizuiwa kuondoka baada ya kushindwa kulipa gharama za hotel pamoja na kukosa nauli ya kurejesha mkoani Mtwara.

Ndanda SC wamemshukuru muimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani kwaajili ya show za tour yake ya kimuziki.

The post Harmonize aiokoa Ndanda SC baada ya kukwama Singida kisa pesa za hotel appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *