Francesco Totti aondoka kwa machungu Roma “Kuondoka hapa nahisi ni bora hata kufa”

Aliyekuwa nahodha wa kikosi cha As Roma, Francesco Totti, ambaye vile vile alikuwa mkurugenzi wa ufundi wa kikosi ameachana na kikosi hicho baada ya kukitumikia kikosi kwa miaka 30 na kuongeza kuwa anajisikia vibaya kuachana na klabu hiyo ambayo aliipenda tangu akiwa kama mchezaji.

Totti ambaye ana umri wa miaka 42 amekichezea kikosi hicho jumla ya mechi 786 na kufunga magoli 307 na kuiwezesha As roma kutwaa ubingwa wa nchini italia (Seria A) mwaka 2001 anaachana na kikosi hicho hasa kutokana na kutoelewana na raisi wa klabu hiyo Jim Pallota.

“Ni kitu kigumu sana mimi kuondoka hapa baada ya kuanza kuitumikia klabu hii kama mchezaji,kuondoka hapa najihisi kama kufa nahisi ni bora hata kufa”.

Wiki iliopita Totti alishindwa kuhudhulia mkutano wa klabu hiyo uliofanyika nchini Uingereza ambapo klabu hiyo ilimpitisha Paulo Sonsera kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo bila mapendekezo ya yeye kama mkurugenzi wa ufundi hali iliopelekea kuonesha kuwa hakuna ushirikiano baina ya Totti na Palloti.

“wanafahamu mitazamo yangu na nini nahitaji ila wamekuwa hawanihitaji kwenye kikosi hiki na mara zote wamekuwa hawanishirikishi katika maamuzi ya klabu hivyo nimeamua kujitenga nao.”

Na Edwini Haule

The post Francesco Totti aondoka kwa machungu Roma “Kuondoka hapa nahisi ni bora hata kufa” appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *