Diamond aachia rasmi video ya wimbo Baba Lao, aonyesha uwezo wake wa kurusha ngumi (Video)

Hatimaye video ya wimbo Baba Lao ya Rais wa WCB, Diamond Platnumz imeachiwa rasmi mchana huu baada ya kusubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa muziki wa BongoFleva nchini Tanzania.

Muimbaji huyo na mfanyabishara siku ya jana aliachia audio ya wimbo huo ambao mpaka sasa hivi una-trend nafasi ya pili katika mtandao wa YouTube huku video ya wimbo Uno ya Harmonize ikishika nafasi ya kwanza.

Katika wimbo huo Diamond ameonekana kurusha vijembe kwa wapinzani wake huku akionekana kupigana boxer ndani ya video hiyo ambayo imeanza kwenda kwa kasi kupitia mtandao wa YouTube.

The post Diamond aachia rasmi video ya wimbo Baba Lao, aonyesha uwezo wake wa kurusha ngumi (Video) appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *