Chris Brown akamatwa na Polisi mjini Paris kwa tuhuma za ubakaji

Mwanamuziki kutoka Marekani Chris Brown amekamatwa na polisi jijini Paris Ufaransa kwa tuhuma za ubakaji.


Imeelezwa kuwa mwanamke mmoja kudai aliwahi kumbaka. Kwa mujibu wa mtandao wa Closer, mwanamke huyo amedai kufanyiwa tukio hilo mapema mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa US. News, Tukio hilo limetajwa kufanyika January 15 – 16 mwaka huu baada ya kikao kwenye kumbi moja ya usiku nchini Ufaransa. Mwanamke huyo (24) alifungua shauri hilo kwa maelezo kuwa Breezy alimualika kwenye chumba cha hoteli ya Le Mandarin Oriental ambapo aliishia kumbaka.

Mmoja wa walinzi wa Brown ni miongoni mwa wengine waliofungwa katika uchunguzi wa Paris, kulingana na afisa huyo. Hakuna afisa aliyeidhinishwa kuwa na jina la umma kujadili uchunguzi.

By Ally Juma.

The post Chris Brown akamatwa na Polisi mjini Paris kwa tuhuma za ubakaji appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *