Cardi B, French Montana na Yo Gotti kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za wizi

Rapper Cardi B, French Montana na Yo Gotti wameshtakiwa na DJ mkongwe nchini Marekani aitwaye,  DJ JMK kwa tuhuma za kutumia beat la wimbo wake bila ruhusa yake.

DJ JMK amesema kuwa ameshafungua kesi kwa mastaa hao, Akidai kuwa French Montana na Yo Got, Cardi B na City Girls walitumia beat la wimbo wake uitwao “Choppa Style” kwenye nyimbo zao za “Oh Yeah” na “Twerk”.

DJ huyo amesema kuwa awali alishafanya mawasiliano na mastaa hao, Na waliahidi kuwa watamlipa lakini mpaka sasa hawajamlipa.

Wimbo wa Choppa Style ulitoka mwaka 2002 na upo kwenye album ya ‘Straight From The N.O” ya DJ huyo. Kwasasa wimbo huo umetazamwa mara milioni 9 kwenye mtandao wa YouTube.

The post Cardi B, French Montana na Yo Gotti kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za wizi appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *