Afisa habari Yanga SC, Dismas Ten aubariki ubingwa wa Simba ‘Bingwa amepatikana, ni bingwa ‘no doubt’, wengine wacha tuone tumekosea wapi’

Afisa habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten amekubali kuwa wapinzani wao wa jadi Simba SC ndiyo mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu huu wa mwaka 2018/19.

Image result for Dismas Ten

Kupitia akaunti yake ya kijamii ya instagram, Ten amesema hakuna ubishi bingwa amepatikana na kilichobaki kuangalia wapi wamekosea.

”Ligi inamalizika kesho, Yes..! Bingwa amepatikana, ni bingwa no doubt..! Wengine acha tuone wapi tukikosea tujipange kwa msimu ujao..!.” ameandika Ten.

Dismas Ten ameongeza ”Ndiyo soccer ilivyo, timu zote zilipambana lakini moja imeupata, hiyo ndiyo maana ya Ligi..!. Nichukue nafasi hii kuwapongeza sana @azamtvtz hakika mmefanya kazi kubwa na ya kiwango cha juu..! Mechi na matukio mengi mmerusha live bila chenga wala mikwaruzo..!.”

”Kupitia ninyi tumeona soka safi kwa mechi za mikoani pia Dar es Salaam, vituko na hata matukio yasiyo ya kawaida yakiwemo yale yaliyoibua mijadala mikubwa miongoni mwa wapenda soka, matukio kama Penalti, offsides, fouls zenye utata nk.”

”Kwenye kila jambo changamoto hazikosi ni vyema kuangalia palipo na mapungufu ili msimu ujao mfanye vizuri zaidi. Ni msimu huu pekee tumeona mechi za Simba na Yanga zikichezwa siku moja kwenye viwanja tofauti na zote kuruka live, awali haikuwahi kutokea….!.”

View this post on Instagram

Ligi inamalizika kesho, Yes..! Bingwa amepatikana, ni bingwa no doubt..! Wengine acha tuone wapi tukikosea tujipange kwa msimu ujao..! . Ndiyo soccer ilivyo, timu zote zilipambana lakini moja imeupata, hiyo ndiyo maana ya Ligi..! . . Nichukue nafasi hii kuwapongeza sana @azamtvtz hakika mmefanya kazi kubwa na ya kiwango cha juu..! Mechi na matukio mengi mmerusha live bila chenga wala mikwaruzo..! . Kupitia ninyi tumeona soka safi kwa mechi za mikoani pia Dar es Salaam, vituko na hata matukio yasiyo ya kawaida yakiwemo yale yaliyoibua mijadala mikubwa miongoni mwa wapenda soka, matukio kama Penalti, offsides, fouls zenye utata nk. . Kwenye kila jambo changamoto hazikosi ni vyema kuangalia palipo na mapungufu ili msimu ujao mfanye vizuri zaidi. . Ni msimu huu pekee tumeona mechi za Simba na Yanga zikichezwa siku moja kwenye viwanja tofauti na zote kuruka live, awali haikuwahi kutokea….! . . Watangazani vijana @baraka_mpenja @pascal_kabombe @hasheem_ibwe @alwatanngoda na wengine Wamekuwa chachu ya kunogesha matangazo yenu…! Hongereni sana @azamtvtz @azamtvtz Hakika ni ‘Burudani kwa wote’ @isco_ten @patrickten_ @nicolasten_ @fadhili_ngoma @matchday_tz

A post shared by Dismas Ten Sylvester (@dismasten) on

Simba ilitarajia kukabidhiwa ubingwa wa ligi hapo juzi kwenye mechi yao dhidi ya Biashara United lakini zoezi hilo likashindikana kutokana na mvua kubwa kunywesha na hivyo kupewa rasmi hapo kesho mkoani Morogoro mbele ya Mtibwa Sugar.

The post Afisa habari Yanga SC, Dismas Ten aubariki ubingwa wa Simba ‘Bingwa amepatikana, ni bingwa ‘no doubt’, wengine wacha tuone tumekosea wapi’ appeared first on Bongo5.com.

Pin It

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *